Pekua/search

Wednesday, November 27, 2013

Kudorora kwa Elimu nchini- Tatizo ni Rais Kikwete au Watanzania?Kudorora kwa Elimu nchini- Tatizo ni Rais Kikwete na Watanzania?
 
Shukuru Kawambwa, Waziri- WEMU
Je Mhe. Rais, ametoa baraka kwa wateule wake (Waziri/Naibu Waziri kwa upande mmoja na Katibu Mkuu wa Wizara) Kutenda kazi kimzahamzaha? SIAMINI!

Inashangaza kuona Katibu MKuu wa Wizara ya Elimu (WEMU) anatangazia umma kuwa muundo wa upangaji wa madaraja na madaraja yenyewe vimebadilika, kisha siku inayofuata Naibu waziri wa wizara hiyo hiyo anapinga habari hiyo mchana kweupe!!! Inashangaza.

Lakini inashangaza na kusikitisha zaidi kuona kwamba inakuwa siku ya kwanza, wiki ya kwanza na ya pili na ya tatu nap engine mwezi....Watu hawa hawajawajibika na hata Mamlaka ya Uteuzi (RAIS) hajawawajibisha.

Naibu waziri WEMU, Mlugo
Inatisha kabisa kuona jinsi tulivyojikalia kimya kama watanzania utadhani hakuna kilichotokea! Tusipoenda barabarani kuhusu hili ni jambo gani litatupeleka huko? Hapa suala ni zaidi ya kuwepo au kutokuwepo kwa hiyo div 5. Suala ni pana zaidi maana linahusu utendaji wa wizara hii muhimu. Maskini sisi!

Pongezi zangu za dhati kwa Nape Nnauye, katibu mwenezi wa CCM kwa kulisema hili wazi wazi kuwa Waziri wa Elimu, with due respect, kazi imemshinda.  Haiwezekani hata kidogo viongozi wakuu kabisa wa wizara moja wakasema mambo yanayokinzana ndani ya wiki moja! Mawasiliano yao yakoje? Na kama ni mabaya, hiyo sio dalili bali ni KUSHINDWA KAZI KABISA!

Bila elimu bora ya ya uhakika Tanzania itakuwa taifa la namna gani? Na bila ya umakini na weledi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  elimu bora itapatikanaje? Inakeraaaaaaa! Inakarahishaaaa!
Katibu Mkuu WEMU, Prof Sifuni Mchome na Kamishna wa Elimu, Prof. Eustella Bhalalusesa

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP