Pekua/search

Saturday, November 30, 2013

Upuuzi wetu kuhusu mgogoro wa CHADEMA



Upuuzi wetu kuhusu mgogoro wa CHADEMA

Wapambe na kina 'nitoke vipi' ni balaa kuliko hatari yenyewe

 
Mbowe, Slaa na Kabwe
Tutakuwa wapuuzi kutarajia kwamba chama cha siasa cha ‘ukombozi’ kama CHADEMA kistawi pasipo migogoro na migongano! Tutakuwa hatuwatendei haki viongozi wa chama hicho na zaidi kutojitenddea haki sisi wenyewe maana tutakuwa tukiishi katika ulimwengu wa kufikirika, ruya ya mchana.

Hata hivyo nadhani ni sahihi kwa wafuasi na au mashabiki wa chama hicho kutarajia mikakati madhubuti ya chama katika kuzuia au kupunguza migogoro na migongano, hususani ile isiyo ya lazima. Ni vema na haki kwa wanachama, wafuasi, mashabiki na wapenda demokrasia kuweka matarajio makubwa kabisa kwa chama kama CHADEMA kuwepo kwa mbinu zenye makali za chama husika katika kutanzua migogoro. Hili ni muhimu maana litaakisi matarajio mapana kwamba iwapo chama hicho kitachukua hatamu za dola, kitafanya vizuri zaidi ya watawala na viongozi waliopo madarakani.

Hapana budi chama chenye kujipambanua kuwa cha mbadala, kikawa na hazina ya busara na weledi unaotakiwa kuibadili  tufani inapoibuka na kuwa utulivu.
 
Kabwe na Mbowe: Kanyaga twende
Hayo yote, mbinu, hekima na weledi yanahitajika sio kwa chama pekee kama chombo bali pia wale wanaojitutua kutaka kushika hatamu za uongozi wa taasisi yoyote kuanzia chama husika hadi taifa. Hapana budi waonyeshe pasipo shaka kwamba wanawazidi wengine kwa mbinu, na busara katika kushughulikia matatizo.

Na busara ya zamani kabisa ya Mfalme Suleimani inatuelekeza kwamba, ni upuuzi usiokifani kuendekeza, “tukose wote”!

CHADEMA na wahusika wote kwenye mtafaruku huu ni lazima wawashinde wapambe na wale kina nitoke vipi! Zitto anao mtihani katika hili, Uongozi wa CHADEMA kwa ujumla unayo changamoto pia. Ni lazima kuwashinda wale wote wanaotaka kujinufaisha na mgogoro huu iwe kwa mali au kutaka umaarufu tu. Wapambe ni hatari kuliko hatari yenyewe. 

Natumaini CHADEMA kitashinda mtihani huu waliojitungia wenyewe.  Nina matumaini makubwa kitaimarika sana. Upepo mkali husaidia sana kujua nakutofautisha matawi imara na yale dhaifu yapukutikayo!
Kila lenye heri tumaini la watanzania! 
Mkumbo na Kabwe

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP