Mauaji ya Dkt. Mvungi- Jambazi Sugu hili hapa
Mauaji ya Dkt. Sengondo Mvungi- Jambazi Sugu hili hapa
Suleiman Kova, Kamanda Kanda Maalum Dar es Salaam |
Jambazi sugu hili hapa, mwaliona?
Limeshiriki kumuua dakta wetu
Sengondo Mvungi, nani atapona?
Huenda na wengine kama Jwani, nani atakana?
Na kujeruhi wengine kama Dkt. Ulimboka, inawezekana!
Ni jambazi sugu hili, licheki
lilivyo pozi, si mwaliona?
Ni jambazi sugu hili lilipohojiwa
limekiri, bila kujibana!
Na limekiri haraka kweli kweli,pasikubishana!
Limejitolea kutuonesha na bastola
ya dakta Mvungi, hakuna kusigana!
Ndiyo, ni lijambazi sugu limekamatwa likiangalia RUNINGA!
Jinale Ngosha, John Mayunga!
Jamani lijembawazi hili si
mmeliona?
Mmelitazama vizuri lakini?
Hilo hapo msijeleta visingizio,
mkadhani ni njama. Ni ujambazi!
Jamani hizi sio ngojera za
kuburudisha tu, sawa?
Bali ni TAMthilia (sema CHUNGU)
iliyosukwa mahsusi, haina dawa!
Msijesema mlizisikia kwa ulimboka
na Yule Mulundi, Mkenya, si ilikuwa
powa?
Msijesema ni zile zile, msijifanye
mmezizoea, mtabishiwa!
Hili ni lijambazi sugu, si lilifungwa?,
Limetoka jela, au mwadhani mahsusi limetolewa?
Ndiyo, hata kama bado halijatoka,
si vibaka walitumwa?.
Vibaka kwa kawaida hawahitaji mali
ama fedha, Mwaelewa?
Hutaka laptop na nyaraka, si ni
vibaraka wenye viraka?
Shenzi zao vibaka wanaopenda kudaka
laptop!
Pumbavu zao vibaka hawa wanaohitaji
nyaraka nyeti
Oh
no! na jambazi sugu lilikuwepo.
Li John Mayunga, Ngosha si la depo!
Tena na baruti zilikuwepo
Hata haya yatapita kama upepo.
Viva Kamanda Kova! Kazi nzuri.
Endelea mpaka mwisho.
Buriani Msomi Mweledi Sengondo Mvungi.
Kwaherini.
Dkt.Sengondo Mvungi, Pumzika kwa Amani |
1 comments:
hilo jamaa ni kiboko ya maboko.
Post a Comment