MOURNING DR. Sengondo Mvungi NO MORE
Sikulilii Tena Dkt Sengondo
Mvungi.
Najililia Mwenyewe na Tanzania hii.
Injili ya Luka 23:
28 Yesu akawageukia, akasema, "Enyi kina mama wa
Yerusalemu! Msinililie mimi, ila lieni kwa ajili yenu wenyewe na kwa ajili ya
watoto wenu. ...
29 Maana, hakika siku zitakuja ambapo watasema: `Heri yao
wale walio tasa, ambao hawakupata kuzaa wala kunyonyesha watoto!`
31 Kwa maana, kama watu wanautendea mti mbichi namna hiyo,
itakuwaje kwa mti mkavu?"
Maandiko yameweka wazi na bayana kabisa. Sina sababu ya
kulia tena. Jana nimekulilia kwa sababu ya ujinga. Nililisahau neno hili.
Mwenzetu Mvungi alikuwa na heri. alipata nafasi ya kujililia mwenyewe. Kumbukumbu zinaonyesha alimwaga chozi hadharani, aliposoma shairi la kumuaga Prof. Jwani Mwaikusa, ambaye naye aliondoshwa kwa mwendo wa aina hii. Alijililia msomi huyu,maana hakujua nani ATAFUATA BAADA YA JWANI.
Mkumbushe chozi hili la Nkurumah, Jwani Mwaikusa.
Iwapo kuna kuonana mpe salaam Nyerere,na Kambona, na Kombe, na Danny Mwakiteleko na wengine na wote wengi!!!
Nenda nenda kamanda.
Tulikuita Kichwa,
Dict alikuita Rodney,
Happy Katabazi, 'Rais Mdhulumiwa',
Sikukufahamu sana.
Vikao viwili vitatu vya kimakakati,
Vimebakisha kumbukumbu mbichi nafsini.
Nenda tu Mvungi nenda.
Mwaondoka wenye kunena,
Wanaondoka wenye kunyamaa,
Ole wangu!!
Tulijua yako thamani,
Tulielewa u mtu makini,
Sikika wanasikika, hawaeleweki
"Huduma za Matibabu ya dharura si Anasa", tunafanya kusudi.
Tulishindwa kukulinda,
Tumeshindwa kukutibu kwa dharula.
0 comments:
Post a Comment