Pekua/search

Saturday, April 5, 2014

TANGANYIKA? I DO NOT LOVE THE NAME

TANGANYIKA, Silipendi Jina hili.

Profesa Shivji
Mwanazuoni nguli nchini Profesa Issa shivji katika kujenga hoja yake dhidi ya utaifa wa Tanganyika anawahoji vijana kwenye kongamano, nadhani na popote walipo,

"Ningependa kujua hapa tulipo ni vijana wangapi kati yenu mlizaliwa kama Watanganyika. Nyoosheni mikono juu. Nyinyi wote mlizaliwa mkiwa Watanzania, utaifa wenu ni Utanzania; utambulisho wenu ni Utanzania; mnajitambua kama Watanzania na mnatambuliwa na wengine kama Watanzania. Ukweli ni kwamba mking’ang’ania Utanganyika wenu, ambao wala hamjui kama mtakuwa mnavunja taifa, mtakuwa mnatumikia maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka."

Lakini najiuliza hivi kweli prof Shivji, hii dhana ya UTAIFA ni iko kwenye jina hili, 'tanganyika' kweli? Mbona katika moja ya hoja zake anafafanua vizuri juu ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar 2010 kuwa neno NCHI limetumika kumaanisha dola!!?

Hapa, kwenye hili la utaifa wa Tanganyika kwa vijana, Mwanazuoni huyu amepiga fallacy na siasa tu. 

Zaidi, hata hii hoja kwamba Taifa la Tanganyika huru lilidumu kwa muda mfupi nayo hoja hii inayo matege ya ki- fallacy na siasa. Kuishi kwa muda mfupi kwa Jamhuri ya Tanganyika hakufuti dhana na mantiki ya utaifa. Mtu ambaye wazazi wake (Biological parents) wamekufa akiwa na umri wa miezi mitatu au chini ya hapo, wale waliomuasili hawageuki kuwa biological parents.

Kwa maana ya jina, mimi nalipenda sana hili jina TANZANIA. Hata hiyo dola ya Tatu kama ingekuja natamani iitwe tu TANZANIA Bara. Hata Muungano ukivunjika, ningependa tu tuitwe Tanzania ama Tanzania Bara. Mbona NBC sio National Bank of Commerce...limebaki kama jina tu!

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP