Pekua/search

Tuesday, April 29, 2014

THE ARAB SPRING: IT IS VERY EASY


Ni rahisi


Ni Rahisi kushutumu na kulaumu upumbavu unaofanywa na utawala wa Misri kutoa hukumu ya kifo kwa mamia ya Wamisri (Muslim Brotherhood)

Ni Rahisi kushutumu na kupuuza nguvu ya umma na kile ilicholeta katika nchi za Misri, Libya, Tunisia nk

Ni rahisi kusahau kuwa hayo ni matokeo ya utawala kupuuza matakwa ya wananchi

Ni rahisi kusahau kuwa mzizi hayo ni hila na danganya toto ya viongozi kwa wananchi

Ni rahisi kabisa kusahau kuwa kiini cha yote hayo ni ubakaji unaofanywa na viongozi kwa fursa zote za wananchi kuamua hatma ya nchi zao

Ni rahisi pia kusahau kwamba hayo yote ni matokeo ya watawala kushabikiwa walipofanya upuuzi kama wa kubaka fursa ya kusikiliza na kufanyia kazi matakwa ya wananchi

Ni rahisi kabisa kudhani yaliyotokea Libya na Misri na kwingineko duniani hayawezi kutokea nchini

Ni rahisi kudhani ukiwaonyesha vifaru na makomando watanzania wataogwaya na kunywea

Ni rahisi sana kusahau kuwa nguvu ya jeshi na mikakati ya ulizi na usalama wake binafsi Muamar Gadaffi ilikuwa kubwa isiyomithilika

Ni rahisi! ni rahisi! ni rahisi kufanya kuwaza na kutenda mambo rahisi


Ni ngumu ni ngumu ni ngumu kujifunza jambo la maana kama kutia maji ukimwona mwenzako akinyolewa.


Saturday, April 26, 2014

Muungano wa Carolight?



Muungano wa Kuupaka karolaiti Hautadumu.


Muungano...Heri kwa watoto wako wanaokiri kuwa umefika umri huu mdogo ukiwa umechoka na dhoofu na mwenye mpauko.


Muungano...heri kwao wana wako wanaokiri na kuamini kwa dhati kuwa kukupaka cream na wakati mwingine KAROLAITI kabisa hakutarejesha uangavu wako mwanana.


Muungano...Heri kwao wana wako ,  wenye tumaini ndani yao kwamba utadumu


Muungano...Heri sana kwao wana wa wewe wenye kuamini kwamba hali hiyo ya udhaifu uliofika nayo leo ni matokeo ya fitina, ujanja ujanja, uongo uongo na hila.


Muungano...Heri kwao wanaopania kutazama yaliyopita kwa jicho kali, kisha kusimama na kutafakari walipokuelemea na kunia kujirekebisha, ili uwe na afya zaidi ukibakiwa na chafya za hapa na pale tu.


Muungano...Heri zaidi kwao wenye kuamini ndani ya nafsi zao kuwa unaweza kupona na kurejea katika afya njema, uwe imara na madhubuti na kusonga mbele miaka 150 ijayo. Ukichanua na nuru yako ikitamalaki tabasamu likitanda usoni pako.


Naam, Heri kwao wenye kuamini kuwa OPERESHENI si kifo. Bali njia ya kukuhuisha maana ukibaki na hayo mawe kwenye figo na donda ndugu tumboni hautadumu.


HERI YA SIKU YA KUZALIWA KWAKO MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR Uliozaa TANZANIA.

Picha zote kutoka blog ya Michuzi

Saturday, April 5, 2014

TANGANYIKA? I DO NOT LOVE THE NAME

TANGANYIKA, Silipendi Jina hili.

Profesa Shivji
Mwanazuoni nguli nchini Profesa Issa shivji katika kujenga hoja yake dhidi ya utaifa wa Tanganyika anawahoji vijana kwenye kongamano, nadhani na popote walipo,

"Ningependa kujua hapa tulipo ni vijana wangapi kati yenu mlizaliwa kama Watanganyika. Nyoosheni mikono juu. Nyinyi wote mlizaliwa mkiwa Watanzania, utaifa wenu ni Utanzania; utambulisho wenu ni Utanzania; mnajitambua kama Watanzania na mnatambuliwa na wengine kama Watanzania. Ukweli ni kwamba mking’ang’ania Utanganyika wenu, ambao wala hamjui kama mtakuwa mnavunja taifa, mtakuwa mnatumikia maslahi na matakwa ya mabeberu na wanasiasa wachache wenye uchu wa madaraka."

Lakini najiuliza hivi kweli prof Shivji, hii dhana ya UTAIFA ni iko kwenye jina hili, 'tanganyika' kweli? Mbona katika moja ya hoja zake anafafanua vizuri juu ya mabadiliko ya katiba ya Zanzibar 2010 kuwa neno NCHI limetumika kumaanisha dola!!?

Hapa, kwenye hili la utaifa wa Tanganyika kwa vijana, Mwanazuoni huyu amepiga fallacy na siasa tu. 

Zaidi, hata hii hoja kwamba Taifa la Tanganyika huru lilidumu kwa muda mfupi nayo hoja hii inayo matege ya ki- fallacy na siasa. Kuishi kwa muda mfupi kwa Jamhuri ya Tanganyika hakufuti dhana na mantiki ya utaifa. Mtu ambaye wazazi wake (Biological parents) wamekufa akiwa na umri wa miezi mitatu au chini ya hapo, wale waliomuasili hawageuki kuwa biological parents.

Kwa maana ya jina, mimi nalipenda sana hili jina TANZANIA. Hata hiyo dola ya Tatu kama ingekuja natamani iitwe tu TANZANIA Bara. Hata Muungano ukivunjika, ningependa tu tuitwe Tanzania ama Tanzania Bara. Mbona NBC sio National Bank of Commerce...limebaki kama jina tu!

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP