Pekua/search

Saturday, April 26, 2014

Muungano wa Carolight?Muungano wa Kuupaka karolaiti Hautadumu.


Muungano...Heri kwa watoto wako wanaokiri kuwa umefika umri huu mdogo ukiwa umechoka na dhoofu na mwenye mpauko.


Muungano...heri kwao wana wako wanaokiri na kuamini kwa dhati kuwa kukupaka cream na wakati mwingine KAROLAITI kabisa hakutarejesha uangavu wako mwanana.


Muungano...Heri kwao wana wako ,  wenye tumaini ndani yao kwamba utadumu


Muungano...Heri sana kwao wana wa wewe wenye kuamini kwamba hali hiyo ya udhaifu uliofika nayo leo ni matokeo ya fitina, ujanja ujanja, uongo uongo na hila.


Muungano...Heri kwao wanaopania kutazama yaliyopita kwa jicho kali, kisha kusimama na kutafakari walipokuelemea na kunia kujirekebisha, ili uwe na afya zaidi ukibakiwa na chafya za hapa na pale tu.


Muungano...Heri zaidi kwao wenye kuamini ndani ya nafsi zao kuwa unaweza kupona na kurejea katika afya njema, uwe imara na madhubuti na kusonga mbele miaka 150 ijayo. Ukichanua na nuru yako ikitamalaki tabasamu likitanda usoni pako.


Naam, Heri kwao wenye kuamini kuwa OPERESHENI si kifo. Bali njia ya kukuhuisha maana ukibaki na hayo mawe kwenye figo na donda ndugu tumboni hautadumu.


HERI YA SIKU YA KUZALIWA KWAKO MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR Uliozaa TANZANIA.

Picha zote kutoka blog ya Michuzi

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP