THE ARAB SPRING: IT IS VERY EASY
Ni rahisi
Ni Rahisi kushutumu na kulaumu upumbavu unaofanywa na
utawala wa Misri kutoa hukumu ya kifo kwa mamia ya Wamisri (Muslim Brotherhood)
Ni Rahisi
kushutumu na kupuuza nguvu ya umma na kile ilicholeta katika nchi za Misri,
Libya, Tunisia nk
Ni rahisi kusahau
kuwa hayo ni matokeo ya utawala kupuuza matakwa ya wananchi
Ni rahisi kusahau
kuwa mzizi hayo ni hila na danganya toto ya viongozi kwa wananchi
Ni rahisi kabisa
kusahau kuwa kiini cha yote hayo ni ubakaji unaofanywa na viongozi kwa fursa
zote za wananchi kuamua hatma ya nchi zao
Ni rahisi pia
kusahau kwamba hayo yote ni matokeo ya watawala kushabikiwa walipofanya upuuzi
kama wa kubaka fursa ya kusikiliza na kufanyia kazi matakwa ya wananchi
Ni rahisi kabisa
kudhani yaliyotokea Libya na Misri na kwingineko duniani hayawezi kutokea
nchini
Ni rahisi kudhani
ukiwaonyesha vifaru na makomando watanzania wataogwaya na kunywea
Ni rahisi sana
kusahau kuwa nguvu ya jeshi na mikakati ya ulizi na usalama wake binafsi Muamar
Gadaffi ilikuwa kubwa isiyomithilika
Ni rahisi! ni
rahisi! ni rahisi kufanya kuwaza na kutenda mambo rahisi
Ni ngumu ni ngumu ni ngumu kujifunza jambo la maana kama
kutia maji ukimwona mwenzako akinyolewa.
0 comments:
Post a Comment