Pekua/search

Monday, May 26, 2014

Dedication to my Heroes- Bishop Amon Dick Mwakisunga

KUTABARUKIA Mashujaa Wangu
Askofu Amon Dick Mwakisunga- Aliyeitwa Kwa Rehema Zake Mungu Kurejea kwake, Mnamo Mwezi kama huu wa Mei 2003 (tarehe 5), Rehema zake Mungu Ziwe Juu Yake.

Katika mengi niliyoweza kujifunza kwa Mpakwa Mafuta huyu wa Bwana ni KUFANYA MAAMUZI. Aliweza kufanya MAAMUZI akapongezwa au Kulaumiwa, lakini Aliamua. Mfano, aliamua kuhamisha Makao Makuu ya KKKT Dayosisi ya Konde kutoka Manow na kuyaleta Tukuyu Mjini. Pale Manow alianzisha shule ya Seminari, ambayo kwa wakati ilianza kuchanua chini ya uongozi wake Baba Mchungaji Mwasamwaja...kabla mchwa haujaingia. Shikamoo mchwa.

Katika ulinganifu mzee wa 'shashaaa' - akimaanisha sasa aliweka mizania kati ya kukuza dayosisi kiroho na kimwili.


Amon Dick Mwakisunga alianza maisha yake akiwa Mwalimu waHisabati, Historia, Jografia na Kiswahili pale Shule ya Misheni ya Kiluteri pale Mwakaleli mnamo Mwaka 1953. Hii ilikuwa ni baada ya kuhitimu elimu yake ya Msingi Manow mwaka 1948, Sekondari pale Bulongwa mwaka 1951 na elimu ya ualimu Rungwe Alliance TTC mwaka 1954.

Kwa upande wa safari yake ya utumishi, alijipatia Stashahada ya Theolojia huko Ujerumani, chuo kikuu cha Hamburg mwaka 1964 na kisha Shahada Takatifu ya Umahiri (Uzamili) chuo kikuu hicho hicho cha Hamburg mnamo mwaka 1967.

Alitumikia katika nafasi mbali mbali ikiwemo kuwa Mkurugenzi wa Vijana wa sinodi ya Kusini ya KKKT, Mhadhiri chuo cha Theolojia Makumira ambapo pia alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo, Katibu wa Afrika huko Geneva katika Fungamano/Shirikisho la Makanisa ya Kilutheri (LWF). Na kati ya Mwaka 1989 hadi 2001 alipostaafu, alikuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Konde. Ndio wakati huu nilipomfahamu mimi.

Pumzika kwa Amani Baba yetu. Wengine sisi hatutakusahau daima.

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP