Pekua/search

Tuesday, August 31, 2010

WAPENDA MAGEUZI SHANGILIENI - USHINDI UMEKUJA

Picha ya wana wa Tanzania wakifuatilia mkutano wa kampeni. Picha kutoka tovuti ya wavuti

When things go wrong as they sometimes will,

When the road you're trudging seems all uphill.

When the funds are low and the debts are high,

And you want to smile, but you have to sigh.

When care is pressing you down a bit,

Rest if you must, but don't you quit.



Life is queer with its twists and turns,

As everyone of us sometimes learns.

And many a fellow turns about,
When he might have won had he stuck it out.

Don't give up though the pace seems slow,

You may succeed with another blow.



Often goal is nearer than

It seems to a faint and faltering man.

Often the struggler has given up,

When he might have captured the victor's cup .

And he learned too late when the night came down,

How close he was to the golden crown.



Success is failure turned inside out,

The silver tint of the clouds of doubt.

And you never can tell how close you are,

It may be near when it seems afar.

So stick to the fight when you're hardest hit,

It's when things seem worst that you mustn't quit.

Shairi hili says it all kwa watawala wanaopuuza nguvu ya umma, wanaobeza uwezekano wa kutokea mabadiliko, wanaoungulia mioyoni lakini wanataka ionekane haiwezekani. Lakini pia ina ujumbe mzito sana kwa wakandamizwa wanaohimizwa kukata tamaa na kuaminishwa kuwa mabadiliko ni ndoto.
Author of this poem is unknown

Saturday, August 28, 2010

ETI HAYA NI MIONGONI MWA MAFANIKIO MAKUBWA YA AWAMU YA JK-


Of all the things, makalio ya mama/dada zetu ilikuwa kipaumbele kumwonyesha Bush siku alipotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juliasi Nyerere Februari 2008.Bongo bwana!Na huendali aliyapenda. 
Ndugu  yangu mmoja hataji mafanikio ya utawala wa awamu hii asipoanza na ujio wa bush nchini. Huwa namsikiliza, maana najua MUNGU AMETUUMBA WENGI. Labda haikuwa kazi rahisi

Friday, August 27, 2010

HUYU NI MIONGONI MWA WENYE VICHWA VIGUMU KAMA ALIVYOSEMA TENDWA?

Tuesday, August 24, 2010

KUMEKUCHA TANZANIA- ILE SAA IMEWADIA?

Dr. Willbrod Slaa CHADEMA presidential candidate
HE.Jakaya  Kikwete, Incumbent CCM presidential candidate

Sunday, August 22, 2010

KUANGUKA KWA JK; JITIHADA ZA KUFICHA KILICHOTOKEA NA KUTELEZA KWA ULIMI

Rais Kikwete akiwa amebebwa. Picha kutoka tovuti ya wavuti

Tulishuhudia TV zikielekezwa kwingine baada ya rais wetu Jakaya Kikwete kupatwa na masahibu viwanja vya jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama cha mapinduzi. Hili labda  lilisukumwa na hofu ya kusababisha taharuki, iwapo mambo mabaya zaidi yangemtokea rais wetu kipenzi (Mungu apishie mbali). Hili sitalijadili zaidi ila ninampa pole mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa masahibu hayo. Kama alivyosema Makamba, Mungu yupo na amjaliye afya tena.
Ninachojadili hapa ni jitihada za baadhi ya magazeti kujitahidi kutolizungumzia kabisa tukio la kuishiwa nguvu na kuanguka kwa rais wetu kipenzi. nitafanya uchambuzi wa gazeti la Nipashe Jumapili. Gazeti hili kwa ujumla halijazungumzia kabisa tukio la jangwani. Hata hivyo, kama wanasaikolojia wanavyozungumzia ‘kuteleza kwa ulimi/ slip of the tongue’ gazeti hili limeishia kutoa msisitizo wa pekee wa kuanguka kwa JK jana.
Kwa maneno rahisi kabisa slip of the tongue ni kukisema kile ambacho kwa sababu moja ama nyingine ‘hakipaswi’ kutajwa. Pamoja na nia ya yeyote au timu yoyote ya gazeti Nipashe Jumapili kutaka kuficha kilichotokea, imeishia kuyamwaga mambo hadharani, indirectly. Hapa pia wanasaikolojia, wanataja sana the power of subconscious mind. Twende pamoja;
kichwa cha Habari kuu kinasomeka; Kikwete: Nitashinda kwa kishindo:
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Hapa neno kishindo linaashiria hamu ya mwandika kichwa hiki kutaka kusema kilichotokea; kutaka kusema ukweli. Je kishindo kipi? Bila shaka ni kishindo cha kiongozi wa watu kuanguka jukwaani.
Kichwa cha habari ya pili kinasomeka; ...CCM yafunika Dar i)
 JK azindua kampeni kwa Kishindo (maana alianguka jukwaani)
ii) Awaambia maelfu: Sitawaangusha (kwa maana ameanguka mwenyewe jukwaani katika siku ya kwanza ya kampeni zake.)
kishindo kimerejewa mara mbili, na kuanguka kumetajwa mara moja, nadhani inatosha kwamba yeyote aliyehusika alikuwa na msongo wa kutosha kutaka kusema kilichotokea kiuhalisia.

Friday, August 20, 2010

MAMBO YAMEIVA UCHAGUZI MKUU- SALA YA WAZALENDO?


Imeitwa - 'sala ya wazalendo'.

"Asante Mungu kwa kuipenda Tanzania hata ukamtuma mwanamapinduzi wa pekee Dr. W. Slaa ili kila Mtanzania atakayempigia kura apate kuleta ukombozi wa kweli.


Tazama umemtuma kwa wapenda haki ili patakatifu (ikulu) pawe na Amani,


Sasa basi Mungu wasaidie watanzania wenzetu wasio na ujuzi wa Kutambua nani kiongozi Bora wamtambue kuwa amekuwa akidai haki zao yapata miaka 15,

Mungu tuepushe na rushwa za vitenge, pombe, simu, na Ahadi za uongo maana wewe hupendi uongo.


NI katika jina la Mungu Baba tunaomba na kushukuru"

Mtunga sala hii: Hajulikani

Monday, August 16, 2010

I AM RESPONSIBLE

“I am responsible. Although I may not be able to prevent the worst from happening, I am responsible for my attitude toward the inevitable misfortunes that darken life. Bad things do happen; how I respond to them defines my character and the quality of my life. I can choose to sit in perpetual sadness, immobilized by the gravity of my loss, or I can choose to rise from the pain and treasure the most precious gift I have – life itself.”

Walter Anderson

TANZANIA HATUJUANI MPAKA TUGOMBEE UONGOZI AU TUTOFAUTIANE NA WENYE MADARAKA

Hussein Bashe 'kada' wa chama tawala, chama dola cha mapinduzi CCM, amezuiwa kugombea ubunge jimboni Nzega, amenyang'anywa uanachama wa chama hicho kwa kuwa 'si raia' wa Tanzania.

Hadi alipogombea na kushinda kura za maoni Bashe alikuwa mwanachama wa CCM na mtanzania safi kabisa. Hivi asingegombea ingekuwaje? Je watu wengine wasio raia halali wa tanzania, ambao hawagombei uongozi inakuwaje? Vyombo vyetu vya usalama na ulinzi wa nchi ikiwemo idara ya uhamiaji, ni vipi?

TUMEZIDISHA 'SIASA'. TUMEENDEKEZA UCHAMACHAMA TUKAENZI MASLAHI YA CHAMA KULIKO TAIFA, TUNASUJUDIA MAKUNDI. TANZANIA IKO SHAKANI. AMANI YETU NI KAMA YA CHURA KWENYE DIMBWI LA MAJI YALIYOTUAMA BARABARANI. TUMEZIDISHA UTANI.

Suala la Bashe limenikumbusha utata wa 'uraia' wa Generali Ulimwengu.

EE MOLA TUNUSURU.

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP