Upuuzi wetu kuhusu mgogoro wa CHADEMA
Upuuzi wetu kuhusu mgogoro wa CHADEMA
Wapambe na kina 'nitoke vipi' ni balaa kuliko hatari yenyewe
Tutakuwa wapuuzi kutarajia kwamba
chama cha siasa cha ‘ukombozi’ kama CHADEMA kistawi pasipo migogoro na
migongano! Tutakuwa hatuwatendei haki viongozi wa chama hicho na zaidi
kutojitenddea haki sisi wenyewe maana tutakuwa tukiishi katika ulimwengu wa
kufikirika, ruya ya mchana.
Hata hivyo nadhani ni sahihi kwa
wafuasi na au mashabiki wa chama hicho kutarajia mikakati madhubuti ya chama katika
kuzuia au kupunguza migogoro na migongano, hususani ile isiyo ya lazima. Ni
vema na haki kwa wanachama, wafuasi, mashabiki na wapenda demokrasia kuweka
matarajio makubwa kabisa kwa chama kama CHADEMA kuwepo kwa mbinu zenye makali
za chama husika katika kutanzua migogoro. Hili ni muhimu maana litaakisi
matarajio mapana kwamba iwapo chama hicho kitachukua hatamu za dola, kitafanya
vizuri zaidi ya watawala na viongozi waliopo madarakani.
Hapana budi chama chenye
kujipambanua kuwa cha mbadala, kikawa na hazina ya busara na weledi unaotakiwa
kuibadili tufani inapoibuka na kuwa
utulivu.
Hayo yote, mbinu, hekima na
weledi yanahitajika sio kwa chama pekee kama chombo bali pia wale wanaojitutua
kutaka kushika hatamu za uongozi wa taasisi yoyote kuanzia chama husika hadi
taifa. Hapana budi waonyeshe pasipo shaka kwamba wanawazidi wengine kwa mbinu,
na busara katika kushughulikia matatizo.
Na busara ya zamani kabisa ya
Mfalme Suleimani inatuelekeza kwamba, ni upuuzi usiokifani kuendekeza, “tukose
wote”!
CHADEMA na wahusika wote kwenye mtafaruku huu ni lazima wawashinde wapambe na wale kina nitoke vipi! Zitto anao mtihani katika hili, Uongozi wa CHADEMA kwa ujumla unayo changamoto pia. Ni lazima kuwashinda wale wote wanaotaka kujinufaisha na mgogoro huu iwe kwa mali au kutaka umaarufu tu. Wapambe ni hatari kuliko hatari yenyewe.
Natumaini CHADEMA kitashinda
mtihani huu waliojitungia wenyewe. Nina
matumaini makubwa kitaimarika sana. Upepo mkali husaidia sana kujua nakutofautisha
matawi imara na yale dhaifu yapukutikayo!
Kila lenye heri tumaini la watanzania!
Mkumbo na Kabwe |