Pekua/search

Tuesday, January 27, 2009

KUBATILISHA LESENI ZA WAGANGA: WANASIASA WETU WATAACHA KWENDA BAGAMOYO, PEMBA, SUMBAWANGA N.K


Enyi wanazuoni weledi,

mwenzenu nauliza tu;
Je ndiyo kusema hatuwaoni tena viongozi wetu wakikimbizana Bagamoyo nyakati za uchaguzi?
Je watavua mapete (yanayohusishwa na imani za kiganga) makubwa makubwa vidoleni mwao?
Je mfumko wa biashara ya vichanga na viungo vya binadamu hospitalini ukitokea, serikali itapiga marufuku utabibu wa kimagharibi?
Je wametumwa na nani na wanataka kumfurahisha nani?
Je tupumue sasa, kwamba maalbino hawauawi tena? Is it an easy n cheap solution to the problem?
Je hatujidhalilishi kama watanzania wenye historia yetu
Je hicho kitengo cha muhimbili kinawathibitisha kwa viwango alivyoweka nani?
Je indigenous knowledge base yetu lazima ifanane nay a kimagharibi?
Kwanini wasishirikishwe? Mbona ni kama wameonyesha ushirikiano mahali pengine?
Motto wa mkulima Pinda anasema kama waganga wa jadi wangekuwa wa kweli na wa uhakika basi magonjwa yangepungua, je hospitali nazozipigwe marufuku? Maana zipo na magonjwa yapo kede kede,
Kwanini mtoto wa mkulima hasemi chochote kuhusu kutotungwa kwa kanuni za kutekeleza sheria ya tiba asilia ya mwaka 2002?

Tumefedheheshwa na dhalilishwa sana na tabia ya wenzetu kuwawinda wenzetu (albino) kama wanyama pori , lakini majibu rahisi rahisi kama hili la serikali, sijui kama yatatusaidia sana . Ningedhani kuwasajili kungesaidia sana kuwajua kuliko vinginevyo!!!

Je baada ya kupiga marufku unafuata msako wa kuwajua iwapo wanaendelea? Kama ndiyo, serikali imeshindwaje kuwakamata waganga wanaowaua au kuchochea mauaji ya albino? NAULISA TU

rejea:http://thecitizen.co.tz/newe.php?id=10084
Ilitolewa wanazuoni yahoo groups

Friday, January 23, 2009

KILA MTU UELEKEO WAKE KUSAKA RIZIKI

Mambo ya Chalinze, hivi karibuni. kila mtu na lake na uelekeo wake

Posted by Picasa

Friday, January 16, 2009

PLAU LINGEWEZA KUKUZA UZALISHAJI KAMA WADAU MBALIMBALI WANGEWEKA MSUKUMO

Teknolojia rahisi ya kulima kwa kutumia jembe la kukokotwa na wanyama ilikuweko na ilithaminiwa zaidi ya miaka elfu mbili sasa. Rejea habari ya Mtu mmoja tajiri kwenye biblia, aliyewaalika watu kwenye karamu.Mmoja kati ya wale ambao hawakufika, alitoa udhulu kwamba, amenunua ng'ombe 'maksai' anakwenda kuwajaribu, hivyo hawezi kwenda karamuni. Pamoja na ukweli huo, teknolojia hiyo haijaweka kuotesha mizizi sehemu nyingi nchini ili walau kuwaokoa watanzania dhidi ya madhila ya jembe la mkono.Pichani mkazi wa kijiji cha Mbambo, Rungwe, ndugu Ndula Mwakipesile ni miongozni mwa wakulima wachache wanaotumia 'plau'. Wakulima wenye majembe ya aina hiyo kwenye kijiji hicho hawazidi watano!! Ni nini msisitizo wa wanasiasa na wanaharakati?

MIAKA 48 YA UHURU, BADO JEMBE LA MKONO!!!!



Mkazi wa kijiji cha Mbambo wilayani Rungwe Mbeya, ndugu Jackson Mwampaka, akipalilia shamba la mahindi, mwisho mwa mwaka jana.

Jembe la mkono ndiyo zana kuu ya uzalishaji miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho sawa na vijiji vingi nchini. Hapo ni karibu nusu karne tangu Uhuru.

TATIZO NI NINI?TUTAOMBA CHAKULA HADI LINI???

NANI KASEMA WATANZANIA SI WABUNIFU??

Mkazi wa Katumba, mjini mdogo pembeni mwa mji wa Tukuyu wilayani Rungwe, ambaye amejichotea umaarufu kwa kuuza sambusa, kababu na ndizi kwenye mabasi yafanyayo safari kati ya Mbeya/Tukuyu na Dar es salaam. Ni maoni ya wadau wengi kwamba biashara yake hiyo 'Inamlipa'. Badala ya kuendelea kubanana na wataalam wenzake wa kutengeneza vyakula hivyo, yeye amebuni utaratibu huo, ambapo anaenda akibadilisha magari. JE ASAIDIWEJE AFANYE VIZURI ZAIDI? NA SISI WENGINE TUFANYEJE, ILI TUTOKE?

Wednesday, January 14, 2009

BENDERA YETU KATIKATI YA MAREKANI NA UINGEREZA KWENYE JENGO LA UMOJA WA MATAIFA, UCHUMI WETU NA USTAWI WETU, MKIANI KWA MATAIFA KARIBU YOTE ULIMWENGUN


INGEKUWA VP KAMA TANZANIA INGEKUWA IMEJIPANGA KIMAENDELEO SAWA NA NCHI INAZOFUATANA NAZO KWA MFUATANO WA MAJINA KATIKA KIINGEREZA??:
1. UNITED KINGDOM
2. UNITED REPUBLIC OF TZ
3.UNITED STATES
Posted by Picasa

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP