Pekua/search

Saturday, June 30, 2012

the Vicious cycle of MIGOMO YA MADAKTARI TANZANIA:


Serikali IMEGOMA. Madaktari WAMEGOMA. Wananchi TUMEGOMA! Hatari tupu






Serikali IMEGOMA kutimiza makubaliano yake na madaktari katika kuboresha huduma za afya


Madaktari WAMEGOMA kutimiza wajibu wao wa watibu wananchi

Wananchi WAMEGOMA  kutumia haki yao na mamlaka yao ya kuiwajibisha serikali kwa kugoma kuboresha huduma za afya sambamba na makubaliano yake na madaktari.

Inabaki kuwa MIGOMO MIGOMO MIGOMO MIGOMOOOOOOO. 

LAZIMA UWEPO UPANDE WA KUANZA KUACHA KUGOMA, SERIKALI!

MADAI YA MADAKTARI:
Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitega alitaja madai yaliyowasilishwa katika kamati hiyo kuwa ni hali bora ya mazingira ya utoaji afya nchini, ongezeko la mishahara, posho za kufanya kazi katika mazingira magumu, posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi na posho za kuitwa kazini.

Akizungumzia dai la hali bora ya mazingira ya kazi, alisema hadi sasa hakuna kilichotekelezwa huku hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa ikizidi kuwa mbaya.

“Tunaweza kusema tangu tukubali kuingia kwenye meza ya majadiliano hali imezidi kuwa mbaya. Katika hospitali kubwa kama Muhimbili inakosa vitendea kazi, dawa, wagonjwa kulazwa chini huku rufaa za wagonjwa kwenda nje ikiongezeka,” alisema Dk Chitega na kuongeza:

“Tunachotaka sisi ni huduma za afya ziboreshwe ili kuwezesha wananchi kupata huduma bora za afya na kupunguza rufaa za kwenda nje kutibiwa.”

Dk Chitega alitoa mfano wa gharama zilizotumika kwa mwaka wa fedha wa 2010/11, kuwa ni Sh7 bilioni, ilhali fedha zilizotumika kwa kipindi cha mwaka huu kwa ajili ya uendeshaji hospitali kubwa sita za hapa nchini kuwa Sh5 bilioni.

“Tulipendekeza pia mchakato wa rufaa uboreshwe kwa kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje kwa kuboresha huduma za ndani, Serikali ilianzisha Taasisi ya Mifupa (MOI), ikapeleka madaktari kwenda kusoma India, wamekuja kufanya kazi wamekosa vifaa wameondoka. Sisi lengo letu ni kuona fedha za nchi zinatumika kuwasaidia Watanzania,” alisema Chitega.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Godbles Charles alisema taarifa zilizotolewa bungeni na Pinda na Dk Mwinyi zimepotoshwa na zina lengo la kuwarejesha kwenye mgomo. CHANZO: http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/24108-madaktari-watangaza-mgomo-kesho


Friday, June 29, 2012

Serikali iliyogoma inapofukuza madaktari waliogoma, wananchi wafanye nini???


KUMBE FUKUZA FUKUZA HII INAWEZA KUTUFIKISHA MBALI EEE

'Hakutakuwa na victimization..lakini ukipigwa na majambawazi au kugongwa na gari usijesema ni silikali, sawa?'

SERIKALI ILIPOGOMA KUTEKELEZA MAKUBALIANO YAKE NA MADAKTARI JUU YA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA IKIWEMO MASLAHI YAO,  NAO MADAKTARI WAKAAMUA KUGOMA KUTUTIBU WANANCHI

SERIKALI INAWAFUKUZA MADAKTARI KWA KUGOMA KUWATIBU WANANCHI
SERIKALI INAWAFUKUZA KWA KUWA IMEWAJIRI MADAKTARI HAO

WANANCHI WAMEKIAJIRI CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) ILI KIUNDE SERIKALI ILIYOWAAJIRI MADAKTARI NA INAYOFUKUZA MADAKTARI KWA KUGOMA KUWATIBU WANANCHI WALIOIAJIRI SERIKALI.

JE WANANCHI WAFANYE NINI NA SERIKALI YA CCM WALIYOIAJIRI?

NAWAZA TU. KIZUNGUZUNGU TU.

Thursday, June 28, 2012

SERIKALI ITATUE MATATIZO SEKTA YA AFYA IACHE VITISHO

  • Iongoze bajeti ya afya
  • Ibane matumizi kwa kuacha kuongeza wilaya na mikoa na ivunje baadhi ya balozi zake nk.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari Dkt Steven Ulimboka akiwa amejeruhiwa vibaya


Kuna taarifa kwamba tayari serikali imeanza kuwafukuza kazi madaktari wanapigania kuboreshwa kwa huduma za afya nchini ikiwa ni pamoja na maslahi yao. Mbali ya kauli za vitisho zilizotolewa na viongozi wakuu wa serikali kuhusu migomo hususan wa madaktari, serikali imeshindwa kusimamia wajibu wake.

Yangu ni machache tu kuwa;
 
  • Wajibu wa serikali ni kukusanya raslimali za nchi ikiwemo kodi na ushuru mbali mbali na kuzitumia raslimali hizo kutoa huduma zote za msingi kwa raia wan chi hiyo. Huduma ya afya ni msingi wa misingi yote.
  • Wajibu wa wananchi ni kutoa hizo kodi, na kuzilinda na kuzitumia kwa uendelevu mali asili zilizopo kwenye maeneo yao.
  • Kwa wataalam, kama madaktari walisomeshwa na serikali, sio kwa hisani bali katika kuwajibika kutimiza wajibu wake(serikali) wanawajibika KUTIMIZA WAJIBU wao na KUPIGANIA KUBORESHWA KWA MAZINGIRA YANAYOHITAJIKA ILI KUTIMIZA WAJIBU WAO.

Serikali ibane matumizi yake na kuachana nay ale yasiyo ya lazima kama kuendelea kuongeza mikoa na wilaya (ukoloni) badala ya halmashauri za wilaya, miji na manispaa (tawala/serikali za wananchi), itimize wajibu wake kwa kutekeleza kile kilichofanya madaktari wakubali kurudi kazini pale awali. Bora serikali ikavunja hata balozi zake nyingine ambazo hazina tija kubwa katika kuiendesha nchi hii (tubaki na zile za kimkakati tu). Serikali itenge bajeti ya kutosha kwa huduma za afya ili kuung’oa mzizi wa fitna. Hakuna njia ya mkato.
Kuwafukuza madaktari ni kuzidi kutoa hukumu ya kifo kwa watanzania tulio wengi. Je kama haina fedha za kutosha kutimiza madai ya madaktari ya kuboresha huduma za afya, itawezaje kutafuta madaktari mbadala ambao wengi ni ghali? SERIKALI IKOME KUTOA VITISHO. WANAWEZA KUMUUA DKT MMOJA, LAKINI HAITAWEZA KUDHIBITI GHADHABU YA WANANCHI INAYOZIDI KUONGEZEKA.

Kwa kuhitimisha niungane na kauli ya Mbunge wangu wa Ubungo John Mnyika,
“Sababu ya hali tete ya nchi na maisha ya wananchi kwenye sekta ya afya ni udhaifu wa serikali na uzembe wa bunge. Rais Jakaya Kikwete ajitokeze alitangazie taifa kuunda tume huru ya kuchunguza kutaka kuuwawa kwa Dk. Ulimboka Steven na kutoa ahadi ya kuongeza fedha katika bajeti ya wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili kushughulikia chanzo cha mgogoro. Spika Anna Makinda aruhusu bunge litumie mamlaka yake ya kuisimamia serikali kusuluhisha.”

Wednesday, June 27, 2012

Je Serikali imemdhuru dkt. steven ulimboka? Soma kauli za viongozi wakuu, tafakari.

Too bad. Pole sana dkt Ulimboka
"...kuna watakaokuja kwenye meza ya majadiliano wakiwa na NGEU na bandeji....."Mwaka 2010 (kama sikosei) Rais Kikwete alipoongelea suala la mgomo wa waalimu

LIWALO NA LIWE..Waziri mkuu Mizengo Pinda leo (Juni 27, 2012) Bungeni Dodoma akiongelea mgomo wa madiwani.

Haya sasa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dkt Steven Ulimboka ameripotiwa kudhuriwa vibaya. Mwana mpole mmoja aliyemshuhudia pale MOI anasema yuko katika hali mbaya sana. Serikali na viongozi hawa wanakwepaje kuhisika? Haya sasa Madaktari waliogoma wataacha kumtibu kiongozi wao?

Sunday, June 24, 2012

WANAJESHI WARUHUSIWA KUWA WANACHAMA WA TANU au ASP

Leo (Juni 24) katika Historia yetu.

Mwaka 1964, siku kama ya leo Serikali ya Tanzania iliwaruhusu wanajeshi kuwa wanachama wa TANU au ASP.

Has this ever been reversed? How non partisan is JWTZ? Tafakari tu usichukue hatua.

Saturday, June 23, 2012

azimio la tanganyika kuwa jamhuri lapitishwa

Benendera ya Tanganyika huru 1961-1964
Leo (Juni 23) katika Historia yetu

Mwaka 1962, Baraza la Taifa lilipitisha sheria ya kuifanya nchi ya Tanganyika kuwa Jamhuri.
kujikumbusha baadhi ya matukio makuu ya nchi yetu bonyeza HAPA au soma zaidi


Chronological History  in Tanganyika
(now Tanzania)
1st Century B.C.                Cushites from Ethiopia settle in Tanganyika.
2nd Century A.D.             Agriculturists from Cameroun and Nigeria settle in Tanganyika and Iron Age Civilization develop.
7th Century A.D.              Arabian merchants settle on the island of Zanzibar off the Tangayikan coast.
10th Century A.D.            Traders from China and India visit Tanganyika in boats on a regular basis.
10th Century A.D.            About this time the fabled emigration of Fijians from Tanganyika takes place.
12th Century A.D.            Swahili Civilization established in Zanzibar and Coastal Area of Mainland Tanganyika.
15th Century A.D.            Organized Kingdoms and Chiefdoms established in various regions of Tanganyika.
1866-1873                         European adventure trips to Tanzania including the visit of Dr.David Livingstone.
1880                                  German Colonization of Tanganyika.
1885                                       Partition of Africa; German Rule of Tanganyika recognized by European powers.
1885-1905                            Wars of Resistance by African tribes against the Germans.
1890                                       British Rule in Zanzibar recognized by major powers.
1914-1918                            British Allies over-run Tanganyika taking the country from the Germans.
1919                                       League of Nations decide to place Tanganyika under British Rule.
1946                                       Tanganyika becomes UN Trust Territory under British Administration.
1961                                       Independence of Tanganyika.
1962                                       Tanganyika becomes a Republic.
1963                                       Zanzibar becomes independent.
1964                                       Union of Tanganyika and Zanzibar to form the United Republic of Tanzania.
1985                                       President Nyerere retires from Office; President Ali Hassan Mwinyi takes over.
1992                                       Multiparty-politics re-established.
1995                                       President Ali Hassan Mwinyi retires and President Benjamin William Mkapa takes over.

Friday, June 22, 2012

SHAABAN ROBERT AFARIKI DUNIA- Leo ktk Historia

Leo (Juni 22) Katika Historia Yetu
 Mwaka 1962, mtunzi maarufu nchini Tanganyika, Shaaban bin Robert  alifariki dunia huko Tanga.Bonyeza HAPA kusoma baadhi ya mashairi yake. Eeeh Mwenyezi Mungu endelea kumrehemu mja wako huyu
















Tuesday, June 19, 2012

WABUNGE NA MAWAZIRI WA CCM WANAVYOTIA KINYAA

Hawa jamaa mawaziri wazima walitoa hela kwa Nchemba kuthibitisha kuwa the House is yet ANOTHER SILLY SEASON!!
"...Kutokana na matusi hayo (ya Nchemba), baadhi ya mawaziri wakiwamo Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo, walimpa fedha Nchemba wakionyesha kuridhishwa na lugha chafu alizokuwa akitoa.

Wakati hao wakitoa fedha hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira na baadhi ya mawaziri, walionekana wakichukua fedha mifukoni kwa kuzikunja kwenye karatasi na kuwapa wahudumu wa Bunge wampelekee Nchemba
"

Soma mwenyewe gazeti la MTANZANIA la leo (Juni 19 2012) Uone upuuzi huu wa wabunge wetu. CCM kinapaswa kupunzishwa jamaniiiiiii kama sio kukizika kabisa. bonyeza HAPA

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP