Pekua/search

Friday, April 27, 2012

HII NI TANZANIA MIAKA 48 BAADA YA MUUNGANO

HII NI TANZANIA MIAKA 48 BAADA YA MUUNGANO

PAMOJA NA HAYO TWAWEZA KUCHEKA PAMOJA - nduhu taabu

Mwalimu Nashoni Mlewa wa shule ya msingi Mwamagembe, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, akiwa darasani (darasa la Sita) shuleni hapo leo hii April 27, 2012.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, bwana Daniel Kaji anasema shule hiyo ina wanafunzi wapatao 312 na walimu sita (ikiwa ni wa kike mmoja). kuna vyumba vinne tu vya madarasa hali inayowafanya wanafunzi wengine kusomea chini ya mti.

Najiuliza hivi ningekuwa mwalimu wa shule hii ningefurahi kufundisha chini ya mti? Ningefanya nini? hivi sasa naweza kufanya nini??? Je mbunge wa eneo hili anaona fahari gani? Mwenyekiti wa kijiji? Diwani? Wananchi wenye dhahabu nyeupe (pamba), mang'ombe na michele kibao, wanajisikiaje? Mkurugenzi wa halmashauri? Afisa elimu na wakaguzi wa shule? Asasi za kiraia, zinajisikiaje? TANZANIA INAGEUKA TANZIA KWA BAADHI YA WATOTO.

Tuesday, April 24, 2012

Serikali ya Kijerumani ilimfuta kazi Karl Peters alipo-misbehave. Haikusema, 'NI UPEPO, UTAPITA.'


Ni Leo (Aprili, 25) katika Historia yetu.

Karl Peters afutwa kazi ya Utawala huko Kilimanjaro.

Licha ya kazi 'nzuri' aliyofanya awali, Serikali ya Kijerumani ilimfuta kazi Karl Peters alipo-misbehave. Haikusema, NI UPEPO, UTAPITA.


Tarehe kama ya leo Mwaka 1897, Mtawala wa kijjerumani katika jimbo la Kilimanjaro, Karl Peters alifukuzwa kazi na serikali yake kutokana na ukatili wake wa kupita kiasi uliochochea migogoro mingi kati ya serikali ya kijerumani na wananchi.

Ikumbukwe hata hivyo kuwa kushamiri kwa utawala wa kijerumani huko Kilimanjaro na nchini kwa ujumla kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na maujanja ya huyu jamaa, Karl Peters, kwa kupiga songi na kuwahadaa watawala wenyeji (machifu) na hatimaye kutiliana sahihi mikataba ya kilaghai (kirafiki). Walipogundua baadaye, jamaa akawageuzia kibao na kuwapiga vita vikali.

Adam Gwankaja Afu ukimwangalia vizuri pichani si anafanana na yule naibu waziri wa JK yule jamaa yuleeeee mwenye kubeba mibinduki miiingi nk nk!!! anapita tu.

Martin Andimile Mbila Mibinduki siyo? Aisee hao jamaa hawana msalie mtume. Ukituhumiwa tu unaondoka haijalishi ni kweli au si kweli. Point ni kwamba watu wameisha poteza imani na wewe na pia ku-waachia wengine wachukue nafasi yako si dhambi maana nao ni binadamu.

Adam Gwankaja kaka Martin Andimile Mbila kuna mengi makubwa ya kujifunza kwa hawa jamaa katika hili kuhusiana na jinsi tunavyojitawala leo hii. Hata Linda Madeleka asiyependa historia (aiogopa) atawafurahia hawa watu. 
The story goes; ukatili wa huyu bwana ulihusisha kuwabaka dada zetu huko uchagani. Na wengine kibao walikuwa wapenzi wake. sasa kama kanuni ya maisha ilivyo mwosha huoshwa, siku ya siku si akakuta mtumishi wake Mabruk anajishindia mmoja wa mahawara wake,Jagodja; weeeee Peters akawaka mbaya. akaagiza washtakiwe kwa WIZI na UHAINI, kisha wakanyongwa na vijiji vyao kuteketezwa. Sasa sikiza hatua za serikali ya kijerumani baada ya kuona huyu bwana anawaharibia. WAKAMFUTA KAZI. Akarudishwa ujerumani huko akapewa kazi nyingine kuacha UCHUNGUZI huru kufanyika. Hii ilikuwa kati ya 1893 na 1895. Ilipofika mwaka 1897 ndipo uchungizi ulipothibitisha tabia mbaya ya huyu bwana, akahukumiwa KUTUMIA VIBAYA MADARAKA, hivyo akafutwa kazi rasmi na kupoteza mafao yake yote. Kesi nyingine zilianzishwa, ila akatorokea zake UINGEREZAAAAAAAAAA. Linganisha na kulinganua na kinachoendelea nchi Tanzania.

Kujiunga na mjadala kwenye FACEBOOK Bonyeza HAPA

Commonwealth Distance Learning Scholarships 2012-2014 for East Africa: apply by 30 April 2012

Commonwealth Distance Learning Scholarships
2012-2014 for East Africa: apply by 30 April 2012

The IOE, in collaboration with the Aga Khan Foundation, is pleased to invite applications for the Commonwealth Distance Learning Scholarships, awarded by the Commonwealth Scholarship Commission in the United Kingdom.
These awards cover the cost of tuition fees for one of the following programmes:
MA in Education and International Development
MA Education, Health Promotion and International Development
MA Educational Planning, Economics and International Development
MA Education, Gender and International Development
Also covered are travel and living expenses for a short period of study in London, from January to March 2014.
Who can apply?
Candidates must be both citizens and residents of Kenya, Rwanda, Tanzania or Uganda.
How to apply
Applications can be made on-line via www.akdn.org. The closing date for applications is 30 April 2012. Please submit the application marked via email to akf.east-africa@akdn.org or via post (marked "Scholarship Opportunity") to:
The Regional Human Resource Manager
Aga Khan Foundation (East Africa)
3rd Floor, The Courtyard
General Mathenge Drive, Westlands
P.O.Box 40898, 00100
Nairobi - Kenya
E-mail: akf.east-africa@akdn.org 
Tel: +254-41 200 5358 / +254 41 200 2879     
Fax: +254-20-212 1805
Please note that applications submitted directly to the IOE will not be accepted; and only short-listed candidates will be contacted.
The deadline is 30 April 2012.

PATA FORM HAPA

Saturday, April 21, 2012

TUNAWEZA HATA KUFUGA FISI - Tunayo maarifa mengi

Tunayo maarifa mengi. Kwanini Hatuendelei kwa kasi zaidi?


Msanii wa ngoma ya asili ya Kisukuma (jina halikupatikana) akionyesha fiisi wakati kikundi chake kilipotumbuiza katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kijiji cha Chela wilayani Kahama Februari 25, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Mjadala kwenye Facebook:


Shununa Isaack kaka adam,asb njema kwanza.huyo jamaa ana kibali chakufuga hujo fisi?au jamaa mambo fulani...

Adam Gwankaja ahsante, na iwe njema sana na kwako dadaangu Shununa Isaack. Hapo sasa kwenye swali lako ndipo tatizo linapoanzia. sheria zetu nyingi ni za kipuuzi sana, maana hazizingatii traditional au ile indigenous knowledge base. Zimeatikwa tu kutoka hukooo ughaibuni. mfano ni Kwanini awe na kibali? Kwani kufuga mbwa twachukua vibali? Usukumani, FISI ni mali aiseee. ha ha ha haaaaaa. Anaweza kuwa mnyama pori au wa kufugwa, upo?? Sikiza sasa wapigania haki za wanyama wenye mrengo wa kimagharibi!!!

Niitiwe Mwansasu Kaka huenda hata siyo fisi, binadamu wana mambo mengi huwawezi!!! Jiulize amempata wapi?

Adam GwankajaNiitiwe Mwansasu, kwani mbwa tunawapata wapi? Hiyo ni indigenous knowldge mwana wane. Usukumani fisi aweza kufugwa bila taabu ujue.

Niitiwe Mwansasu Wenye kwao watanisamehe lkn Dom wanafuga punda ila kwa baadhi ni kitoweo na kuwasaidia kubeba mizigo!! Sasa anawasaidia nini km co mambo fulani....???

Adam Gwankaja ha ha haaaaa dadaangu weye!!!! hata hayo mambo flan ni maarifa, ila ukristo ulipkuja ukatuharibia sana, na tukazidi kuyaficha; tukayaficha yale distructive na constructive kwa pamoja. moja ya matumizi ya fisi huku naambiwa ni USAFIRI!

Shununa Isaack nakubaliana nawewe kaka adam.makatiba yetu sio.watuache tujifugie manyoka,fisi nk.mi ntafuga tembo na jamaa simba.niwaone wezi.pia siku navuna meno yangu ya tembo nisione mtu anasogea.pia kaka wale swala ntafuga kwa wingi kila siku kamoja kanaliwa.upo hapo vyetu bwana

Niitiwe Mwansasu Mpendwa wangu hayo mambo fulani yana faida gani kwetu? Mbona tunazidi kuwa masikini wa kutupwa! Makubwa usafiri wa fisi unakuwaje? Jamani hebu wamkumbuke mungu kwanza ili awasaidie!!!

Adam Gwankaja Ha ha ha haaaa ushaanza fujo zako Shununa Isaack dadaaangu. Tamaduni ni muhimu. majuzi hivi nilikuwa Nepal huko mashariki chini ya Himalayas, nimestaajabu wanafuga tembo ujue. Hana fujo wala nini. Ziko nchi nyingine wanafuga mbogo/nyati ujue.

Adam GwankajaNiitiwe Mwansasu kwa hali iliyomo leo baada ya uharibifu uliofanywa na ukoloni na utamaduni wao, nakubaliana na wewe. Lakini tumekosea sana kudhani kila maarifa asilia ni dhambi. sio kweli. mfano mdogo, wamisionari waliwakataza wazee wetu hata kutumia mitishamba, leo wamerudi na products za miti ile ile (alovera kwa mfano) wanatufundisha kuitumia. So nalitazama suala hili kwa upana namna hiyo. Kwamba yako maarifa yetu yanapotea, na kuzidi kupotea.

Kujiunga na mjadala: bofya HAPA

Friday, April 20, 2012

PUMZIKA KWA AMANI BRIGEDIA JENERALI ADAM MWAKANJUKI

Nenda Brigedia Jenerali (Mstaafu) Adam Mwakanjuki. Pumzika kwa amani. Mbio ulizipiga, nchi uliijenga. Utabaki KUWA mfano na ushuhuda wa MUUNGANO wetu. Pumzika kwa amani baba yetu




Picha imesombwa kutoka: http://www.mjengwablog.com.

PORI LA SERENGETI LA GEUZWA HIFADHI YA TAIFA

Leo (Aprili 20) Katika Historia Yetu

Mwaka 1948 Mbuga za Pori la Serengeti, zilifanywa kuwa Hifadhi ya Taifa.

Mungu kaijaalia nchi hii wingi wa utajiri, kila aina ya utajiri. 

Wednesday, April 18, 2012

PONGEZI MARUBANI WA PRECISION AIR KWA KUTANGAZA UTALII

PONGEZI MARUBANI WA PRECISION AIR: Mkandawile, Anderson Wililo na Focus Mbaga

Ni vema, haki na wajibu KUWAPONGEZA Marubani wa PRECISION AIR (PW) Mkandawile, Anderson Wililo na Focus Mbaga, ambao wanakwenda zaidi ya hatua ya matangazo ya kawaida.... 'cabin crew sijui nini na nini cruising wapi na wapi'. Ndugu hawa WANATANGAZA UTALII ILE MBAYA.

Utasikia ...On your left is mount Kilimanjaro, the highest mountain in Africa..YOU SHOUlD BE ABLE TO SEE THE BEAUTIFUL SNOW CAP, Thats Kibo, sijui Mawenzi peak... mara sijui Bagamoyo is historic town, mara sijui spend some time in Arusha, sijui mount Meru is what and what, mara Serengeti and Ngorongoro whatsoever. Wameonyesha mfano ndugu hawa, HATUNABUDI KUWAIGA KILA MMOJA WETU KATIKA AFANYALO AWEKE UZALENDO MBELE.


Mjadala kwenye FACEBOOK bonyeza HAPA

Tuesday, April 10, 2012

KIFO CHA KANUMBA NA MAPENZI YETU KTK KIFO NA SIO UZIMANI



Oh Steven Kanumba, how I wish tungekuonyesha 'upendo huu' ukiwa hai! Kuondoka kwako mapema hivi kumeniachia maswali mengi;


Je watanzania tutaendelea kupenda marehemu zaidi kuliko waliohai mpaka lini? Je michango ya mamilioni eg milioni kumi aliyotoa Rais itafanya kazi gani? Italiwa tu, kunywewa tu na kisha KUNYA na KUKOJOA?

Je itakusanywa na kuanzisha STEVEN KANUMBA FOUNDATION ili kuyaendeleza mawazo yako?

Oh nalia mie, ila siji msibani. WACHA NIJIULIZE TU.


Soma mjadala kuhusu hii kwenye FACEBOOK, bonyeza HAPA

Saturday, April 7, 2012

WOSIA WA STEVEN KANUMBA

Yaweza kuwa yako mengi mazito yaliyotendwa, kunenwa na Steven Kanumba sambamba na yale ya kimtazamo. Nimechagua ujumbe huu kuwa WOSIA wa Kanumba kwa Watanzania. Kwangu unaonesha kuwa alikuwa zaidi ya tuliyemwona jukwaani.

Ameongelea uzalendo na kupendana, kujithamini kama watanzania na kuthamini chetu nk. Sikiliza undani wa maneno yake HAPA
au fuata kiunganishi hiki cha Youtube http://www.youtube.com/watch?v=NIsJd2MF56w&feature=related

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP